WAZIRI AWESO AIPONGEZA TANGAUWASA KWA KUFANIKISHA MAUZO YA 103% YA HATIFUNGANI YA KIJANI
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso ameipongeza Mamlaka ya Maji jijini Tanga(@tangauwasa) kwa kufanikisha mauzo ya asilimia 103 ya Hatifungani ya Kijani ya miundombinu ya maji Tanga ambapo zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 54.72 zimekusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwa matarajio yao yalikua Shiling Bilion 53.12.
Aweso amesema wazo hilo lilikuwa la Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan(@samia_suluhu_hassan) mnamo tarehe 22 mwezi February 2024 alipowakilishwa na Mhe.Makamu wa Rais Dkt.Philip Isdor Mpango (@dr_philip_isdor_mpango) katika uzinduzi wake.
.
"Haya ni mapinduzi makubwa sana katika sekta yetu ya maji yenye lengo la kufanikisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi, kwa hakika sekta ya maji imeandika historia mpya Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kwa ubunifu huu.
.
"Mwanzo jambo hili lilionekana haliwezekani lakini niliwasisitiza tuthubutu na tutaweza na hakika tumeweza,Fedha hizi zilizopatikana zinaenda kuwezesha utekelezaji wa miradi ya kimakakati ya kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa wakazi wa Tanga Jiji pamoja na Miji ya Muheza, Pangani na Mkinga sambamba na kuimarisha usimamizi na utunzaji wa vyanzo vya maji" alisema Aweso.
Aidha, Waziri Aweso ametoa Shukrani kwa Mhe.Rais Dkt.@samia_suluhu_hassan kwa kununua Hatifungani hiyo na wadau wote walioshiriki katika ununuzi wa Hatifungani ya TangaUWASA na hongera kwa Mbunge wa Jimbo la Tanga Mhe.Ummy Mwalimu.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

