MIAKA 60 YA MUUNGANO, ZIMAMOTO INAKWENDA KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA HAPA NCHINI - WAZIRI MASAUNI
Serikali imejipanga kufanya mageuzi makubwa na ya kisasa katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kuondoa malalamiko ya uhaba wa vifaa pale yanapotokea majanga.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni leo April 15,2024 alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Wizara katika Kipindi cha miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ukumbi wa jengo la LAPF jijini Dodoma.
Masauni amesema mwaka huu 2024 wamenunua magari mapya 12 ya kisasa ambayo yanatoka nchini Australia, na tayari yameshafika hapa nchini, na uzinduzi wa magari hayo wamepanga kufanya ndani ya sherehe ya miaka 60 ya Muungano, ambapo uzinduzi huo utaenda sambamba na uzinduzi wa nyumba za askari wa Zimamoto za kisasa Kikombo Jijini Dodoma na vituo vya Zimamoto vya kisasa.
.
"Mwaka huu Mwezi wa 11 tunatarajia kupokea vifaa vya kisasa vya awamu ya kwanza kwa ajili ya Jeshi la Zimamoto, Rais Samia ametoa Dola milioni 100 ili tuweze kuondokana na malalamiko ya uhaba wa vifaa katika Jeshi letu" alisema.
.
Waziri Masauni amesema uwekezaji huo unahusisha Magari 150 na kila mkoa na wilaya utapata gari zaidi ya moja, na pia uwekezaji huo unahusisha boti 25 za kisasa za Uokoaji na Uzimaji moto,na helikopta maalum kwa ajili ya kuzima moto.
.
Mhandisi Masauni amesema katika Kipindi cha miaka 60 ya
Muungano,wamepanga kutoa elimu kwa askari wa Zimamoto ili waweze kuwa na weledi wa kutumia mitambo ya kuzimia moto na kuongeza idadi ya askari wa Jeshi la Zimamoto hapa nchini.
.
"Kwa hivi Sasa kuna askari wanakwenda mafunzoni na bajeti ya mwaka huu tunataka kuomba kuongezwa askari wengine ili tupate vijana ambapo watakuwa wamepata mafunzo vizuri kutumia vifaa hivi kwa uweledi" alisema Mhandisi Masauni.
.
Aidha, Waziri Masauni ametoa wito kwa watanzania wote kutii Sheria za nchi kwani hakuna mtu yeyote atakaye vunja sheria za nchi na Serikali italifumbia macho suala hilo halikubaliki kabisa.
@wizaramnn
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

