TEMESA WAASWA KUONGEZA UBUNIFU KATIKA MAENEO YAO YA KAZI
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amewataka watendaji wa Wakala wa Ufundi Na Umeme Tanzania (TEMESA) kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na kuwa wabunifu katika kuanzisha vyanzo vipya vya mapato.
.
Mhandisi Kasekenya ameyasema hayo leo Machi 18,2024 alipokuwa akifungua Kikao Cha Baraza la Wafanyakazi TEMESA jijini Dodoma.
.
Kasekenya amesema kazi nyingi zinazofanywa na Wakala huo,baadhi ya wateja wao wamekuwa hawaridhiki nazo hivyo wanapaswa kuwa wabunifu ili kupunguza malalamiko ya wateja wao.
.
"TEMESA kwenye baadhi ya mikoa inafanya vizuri na baadhi ya mikoa haifanya vizuri,Mimi nikiwa kama Naibu Waziri mara kadhaa katika kamati ya miundombinu tumeona wajumbe wakiwa hawaridhishwi sana na baadhi ya shughuli zetu tunazozifanya, lakini kama tutatambua dhamana yetu ambayo Serikali imetupa tuna dhamana moja muhimu sana.
.
"Chombo cha TEMESA kimekuwepo kwa sababu sisi ni watumishi wa umma ambao moja ya kazi yetu kubwa ni kuhakikisha kwamba magari yote ya Serikali yakiwepo ya viongozi yanatengenezwa na Karakana za TEMESA, kwahiyo mjitoe na kuwa wabunifu na waaminifu"alisema Mhandisi Kasekenya.
.
Naibu Waziri Kasekenya amesema Ofisi nyingi za TEMESA zilizopo mikoani hazipo kwenye hali nzuri ya kimazingira hivyo wanapaswa kubadilika ili kujenga taswira nzuri kwa watu hapa nchini.
.
Kwa Upande mwingine,Kasekenya amewataka watendaji hao kujadili suala la bei ya utengenezaji wa magari ya wateja wao kwani wamekuwa wakilalamika kwamba imekuwa ni kubwa mno.
.
Aidha, Mhandisi Kasekenya amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi wa TEMESA kukaa na mafaili ya wafanyakazi wao kwa muda mrefu ofisini,hivyo amewaomba waweze kulijadili suala hilo katika kikao.
.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Ndg.Lazaro Kilahala amesema mpaka hivi Wakala huo umekamilisha usimikaji wa mfumo wa kusimamia mapato yanayokusanywa kupitia POS,mfumo wa madeni TEMESA, mfumo wa ukusanyaji mapato (N-CARD), uboreshaji wa mfumo wa mapato Kigongo- Busisi.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

