logo

JENGO LA WIZARA YA MAJI LITACHUKUA WATUMISHI WASIOPUNGUA 455 - WAZIRI AWESO

Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso(@jumaa_aweso)amesema jengo la Wizara ya Maji linalojengwa jijini Dodoma katika Mji wa Serikali Mtumba limekamilika kwa asilimia 99.

.

Aweso ameyasema hayo alipokuwa ametembelea na kukagua jengo hilo lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

.

Amesema jengo hilo la kisasa lina ghorofa sita, vyumba 281 na lina uwezo wa kuchukua watumishi wasiopungua 455.

.

"Pia jengo hili lina kumbi 12 za mikutano ukiwemo ukumbi mkubwa wenye uwezo wa kuhudumia watu 155" amesema Waziri Aweso.

.

Waziri Aweso amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake katika kuhakikisha majengo ya Wizara mbalimbali katika mji wa serikali yanakamilika ikiwa ni pamoja na jengo la Wizara ya Maji katika kuhakikisha wafanyakazi wa Wizara ya Maji wanafanya kazi katika mazingira mazuri.

Kwa upande mwingine, Waziri Aweso amewataka watendaji wa wizara hiyo kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ili kuhakikisha huduma ya maji inamfikia kila Mtanzania kama Serikali ilivyopanga kuwahudumia wananchi katika suala la huduma ya maji.

Aidha, Katika hatua nyingine amempongeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji @eng_mwajuma.waziri9 ambaye ndiye msimamizi mkuu wa Ujenzi wa Jengo hilo kwa kazi kubwa na nzuri aliofanya yeye pamoja na timu nzima ya mainjinia wa @wizarayamajitz.

"Nimemshukuru Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa na ofisi yake kwa kazi kubwa ya uratibu wa ujenzi huu wa mji wa serikali mtumba Dodoma ambapo kazi katika maeneo mbalimbali inaendelea kwa kasi" amesema Aweso.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn