KENYA YAPANGA KUPITISHA SHERIA YA TOHARA YA LAZIMA KWA WANAUME KUANZIA UMRI WA MIAKA 0-18
Mswada mpya umewasilishwa mbele ya Bunge la Kitaifa la nchini Kenya, unaotaka kufanya Tohara ya lazima kwa wavulana wenye umri wa miaka 0-18, lakini chini ya usimamizi wa wahudumu wa afya waliopata mafunzo vyema ya kitabibu.
.
Mswada huo unaopendekezwa na Mbunge wa Mukurweini Ndg.John Kaguchia umesema kuwa, utekelezaji wa mswada huo utapunguza kwa kiasi kikubwa kuenea kwa Magonjwa ya Kujamiiana(STDs).
.
Mswada pia unataka Tohara ya kitamaduni ipigwe marufuku na nafasi yake kuchukuliwa kikamilifu na kata iliyoidhinishwa kimatibabu, ambayo ni lazima kwa wanaume wanaozaliwa hadi umri wa miaka 18, na hivyo, kuiondoa kutoka kwa mila na desturi hadi hitaji la afya ya umma.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

