RAIS SAMIA ATOA MAAGIZO WIZARA YA ULINZI "KAMBI ZOTE ZA JKT ZIREKEBISHWE
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Ameitaka Wizara Ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kuandaa Mpango Mkakati Wa Kurekebisha Makambi Yote Ya JKT Kwa Kuanzia Upande Wa Malezi Ya Vijana Ili Serikali ijielekeze Huko.
.
Samia Ameyasema Hayo Leo Julai 10,2023 Alipokuwa Kwenye kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
.
Amesema Wizara Hiyo inatakiwa Kuiwezesha SUMA JKT Ili kuweza kuingia kupata Mikopo Ili wazalishe na Hapo Baadae Waweze Kurudisha Mikopo Na Shirika liweze kusonga Mbele.
.
"Kama itatakiwa Udhamini Wa Serikali Au Vyovyote Serikali Tupo Tayari Kuwezesha SUMA JKT Ili iweze Kuzalisha Kwa Kiwango Kikubwa" Amesema Samia.
.
Rais Samia Amesema wanakwenda Kuunganisha Mpango wa Programu ya BBT na Kinachofanyika JKT Ili Vijana wawe na Muelekeo Mzuri.
.
"Tunaposema Tunakwenda kukarabati Makambi Zaidi, Na Makambi yanayokwenda Kurekebishwa mbali na Mafunzo ya Ukakamavu Na Kijeshi yataungana na Mpango wa BBT Ili kuwajengea Kesho nzuri Vijana na wakishamaliza wajue wanakwenda wapi na Kufanya Nini" Amesema Samia.
Aidha, Rais Samia Amesema Mafunzo Yanayotolewa Na Jeshi Hilo yawasaidie Vijana Kuwa wazalendo Wa kweli wanaothamini Utaifa,Umoja Na Mshikamano Wa Watanzania.
.
Kwa Upande Wake Waziri Wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mhe.Innocent Bashungwa Amesema Mafunzo Ya JKT ni Sehemu Muhimu ya Mchango Wa Amani tuliyonayo Tanzania, Wizara Itaendelea Kushirikiana Na wizara Za Kisekta Kuboresha Mafunzo Stadi za Kazi Kwa Vijana Wa Jeshi la Kujenga Taifa na kuwawezesha Kwa kuwapatia Ujuzi na Maarifa Zaidi ya Ilivyo Sasa.
.
Naye Mkuu Wa Majeshi ya Ulinzi Na Usalama Jenerali Jacob Mkunda Amelitaka Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) kuzifanyia Changamoto Hizo wanazokumbana nazo kama Fursa Ya Kufanya Ubunifu na Kuweka Mikakati ambayo Itawezesha Kutekeleza Majukumu Yao Kwa Ufanisi stahiki.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

