JKT YAWAKUTANISHA MAVETERANI KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 60
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limeombwa Kuhakikisha linaandaa Mabonanza Mbalimbali Ya Vijana Ikiwemo na Kumiliki Vituo Vya Kukuza Na Kulea Vipaji Kwa Lengo La Kupata Wachezaji wengi wazawa Wenye Vipaji na Kuepukana Na wimbi Kubwa la Wachezaji Wa Kigeni wanaokuja kuchezea Timu zetu hapa Nchini.
.
Ombi Hilo limetolewa na Aliyekuwa Mchezaji Wa Zamani Wa Timu Ya Taifa Stars Bw.Lubigisa Madata Leo Julai 08,2023 Alipokuwa Kwenye Bonanza La Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lililofanyika Katika Uwanja Wa Kilimani CLUB Uzunguni Jijini Dodoma Kuelekea Kilele Cha Maadhimisho Ya Miaka 60 Ya Jeshi la Kujenga Taifa.
.
Amesema Yeye anaamini JKT Wana Uwezo mkubwa Sana Na endapo itatokea watatengeneza Academy Kubwa Ya itakuja Kufanya Vizuri Sana Na pia Itatoa Vipaji Vingi Hapa Nchini.
.
"Moja Kati Ya Wachezaji wao JKT ni Vijana Na Hata wanaokuja Kujiunga Na Jeshi Bado Wana Umri mdogo Sana hivyo wanaweza wakawachukua na wakaenda wakapata Kazi wakacheza na Bado tukawa na Vizazi Vizuri. Kwa Sababu hivi Sasa Timu ya Taifa kama ukiangalia utaona inatoka Nafasi kwa kuchambuliwa, kwahiyo kama JKT watazalisha huku Chini tutapata Wachezaji wazuri Zaidi" Amesema Lubigisa.
.
Kwa Upande Wake Mkurugenzi wa Mawasiliano Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Juma Issa Mrai Amesema Bonanza Hilo ambalo limekutanisha Watu Mbalimbali Ikiwemo Wananchi Na watumishi wa Jeshi la Kujenga Taifa linakuza Ushirikiano Baina Yao Na Kukuza Upendo.
.
"Zamani kulikuwa Na Dhana ya Kwamba Watu Wanaogopa Wanajeshi Lakini Sehemu kama Hii mnapokutana ndio Kutoa Dhana hiyo ya Kwamba Jeshi halichangamani na Watu wengine Hapana,Huu ni Upendo Tu" Amesema Kanali Mrai.
.
Bonanza Hilo limezikutanisha Timu za JKT Veterani Na Twalipo Veterani Ambapo Mchezo Wa ufunguzi Wa Mashindano ulimalizika Kwa Sare ya Magoli Mawili Kwa Moja.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

