logo

JAMII YATAKIWA KUIUNGA MKONO TUMAINI FOUNDATION ILI WAWEZE KUTIMIZA MALENGO YAO

MRATIBU wa Elimu maalum Kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi Na Teknolojia Bw.Leonard Henelico Ameitaka Jamii Na Watu Mbalimbali Kwa Ujumla kuiunga Mkono Taasisi inayosaidia Watoto Wenye Mahitaji Maalum Ya 'Tumaini Foundation' Ili Kuhakikisha Kwamba Yale Malengo ya Msingi waliyojiwekea au waliyoyakusudia kuyapata Basi Wanafanikiwa Kuyapata Kwa Urahisi Ili kuweza Kusaidia Watoto hao.

.

"Tuwaunge Mkono Kwa Njia Mbalimbali hata Rasilimali Nk. Kwa Sababu Kuwasaidia Watoto 350 Sio Jambo dogo nawapongeza Tumaini Foundation"

.

Henelico Ameyasema Hayo Leo Juni 24,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Kwenye Kilele Cha Programu Maalum ya Kuwapeleka Watoto Shule Bila Kujali Maumbile Yao ambapo iliambatana Na Tukio la Kuendesha Baiskeli Katikati ya Jiji Hilo.

.

Henelico Amesema Kupitia Wizara ya Elimu Wameamua Kujenga Shule Jumuishi Za Mfano Nchi Nzima na Kwa Kuanzia wamejenga Shule Ya Sekondari Patandi, ambayo inapokea Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum, Shule Ya Msingi Luguleni iliyopo Masasi, Nguye iliyopo Mkoani Geita.

.

"Kwa Sasa Tuna Shule 3 za Mfano Na Malengo Yetu Kuhakikisha Kwamba Kila Kata inakuwa na Shule Maalum Ya Mfano Na Baadae Kila Mkoa kutakuwa na Shule Maalum Ya Mfano Na Hatimaye Kila Halmashauri inakuwa ya Mfano" Amesema Mratibu Huyo.

.

Mratibu Huyo Amesema Watoto Wenye Mahitaji Maalum Hasa Wenye Ulemavu Wote wanaweza Kujifunza Na Kitu Cha Msingi Ni Kwamba inatakiwa kuhakikisha wanawatengenezea Mazingira Rafiki ya Kujifunzia.

.

"Mtoto mwenye ulemavu anaweza akajifunza, Kitu ambacho kinaonekana ya Kwamba hawawezi ni ule Mtizamo Potofu. Kwa Kweli Suala La Kujifunza Ni Suala la Mtu Mmoja kwahiyo Kila Mwanafunzi anaweza Kujifunza Kwa Kiwango na Kasi Yake.

.

"Kwahiyo tunaendelea Kutoa Maelekezo Kwa Walimu Wote Ili waweze Kujua Namna Bora Ya kuhudumia Hawa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum Katika Madarasa Yetu ya Kufundisha" Amesema Henelico.

.

Aidha, Henelico Amesema Kila Halmashauri Ina Afisa Elimu Wa Mkoa hivyo amemshauri Mkurugenzi Wa Tumaini Foundation Bi.Tumaini Kivuyo Kuwa Nao Sambamba Ili waweze Kumshauri Kwa hili na Lile, Na Kwa Yale yatakayoshindikana Katika Halmashauri wao kama Wizara wapo tayari Kutoa Ushirikiano Kwake Ili waweze kumsaidia.

.

Aidha, Henelico Ameipongeza Taasisi hiyo Kwa Kusapoti Watoto Wenye Mahitaji Maalum Katika Nyanja Mbalimbali Ili waweze Kupata Elimu Kwa Maisha Yao Ya Baadae.

.

Mkurugenzi Wa Taasisi Hiyo Amesema Mpaka Sasa hivi Taasisi Hiyo inahudumia Watoto 350 Nchi Nzima, Na Kati Ya Watoto, Watoto 50 wanaishi Na Mahitaji Maalum na Tofauti Tofauti.

.

Kivuyo Amesema Changamoto wanazokutana nazo Katika Taasisi Yao kwenye Ili Kutimiza Elimu ya Watoto Jumuishi Ni Unyanyapaa, Tamaduni Potofu zinazoonekana Watoto hao hawawezi Kufikia Ndoto Zao.

.

"Ninatoa Shukrani Zangu Kwa RAIS Dkt.Samia Suluhu Hassan Kwa kuipa Kipaumbele Elimu Pamoja na Mawaziri Wote wanaohusika na Eneo hili la Elimu.

.

"Naiomba Serikali iweze Kutilia Mkazo Katika Elimu maalum Na Hasa Elimu Jumuishi" Amesema Kivuyo.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn