logo

WAGONJWA WANAOTOLEWA MAWE KWENYE MFUMO WA MKOJO SASA KUKAA WODINI SAA 24-BMH

Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa wa mfumo wa mkojo Okoa Sukunala wakati wakiendelea na matibabu ya kuondoa mawe kwenye mfumo wa mkojo katika kambi maalumu inayo endeshwa na madaktari bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya ACIBADEM ya nchini Uturuki

‎"Hospitali ya Benjamin Mkapa ina vifaa vya kisasa vinavyo wezesha kufanya matibabu ya kutoa mawe kwenye mfumo wa mkojo bila kufungua mwili ni kwakutumia matundu madogo (laparoscopic)" alisema Dkt. Okoa.

‎Ameongeza kuwa kuna faida nyingi za kutumia teknolojia hii ya matibabu

‎"Faida ni nyingi lakini nieleze moja kubwa ambayo inamuondolea adha mgonjwa akishafanyiwa matibabu haya atakaa wodini kwa muda usiozidi masaa 24, ambapo awali ilikuwa inamlazimu kukaa wodini siku tano" alisema Dkt. Okoa

‎Hospitali ya Benjamin Mkapa inaadhimisha miaka kumi ya utoaji huduma huku ikiendelea kuboresha huduma zake huku ikijikita katika matibabu ya teknolojia ya hali ya juu

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn