logo

MTOTO WA TEMBO ALIYENASWA NA MTEGO WA MAJANGILI AOKOLEWA KANDO YA MTO RUHUDJI MKOANI MOROGORO ‎

Timu ya wataalam wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) wakiongozwa na Dkt. Richard Samson wamefanikiwa kumuokoa mtoto wa tembo aliyekuwa amenaswa na mtego wa majangili kando ya mto Ruhudji katika pori la akiba la Kilombero lililopo wilayani Malinyi mkoani Morogoro takribani kilomita 400 kutoka Manispaa ya Morogoro.

‎.

‎Mtego huo, uliotengenezwa kwa kamba yenye nguvu, ulikuwa umekamata mguu wa mbele wa tembo, na kuhatarisha maisha yake na kusababisha maumivu makali.

‎.

‎Uokoaji huo ulifanyika kwa ushirikiano na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inayosimamia Hifadhi ya Wanyamapori ya Kilombero ikiwa ni juhudi za pamoja za kuimarisha uhifadhi na kuhakikisha usalama wa wanyamapori hao.

‎.

‎Wataalamu wa SUA na TAWA waliweza kuokoa afya na uhai wa tembo huyo mdogo kwa kumtoa kamba iliyokuwa imemfunga mguu wake wa kulia kwa muda wa siku mbili hali iliyomfanya mnyama huyo kushindwa kutembea wala kupata chakula na maji.

‎.

‎Operesheni hii ni mfano wa mafanikio ya uhifadhi na mipango ya afya ya wanyamapori iliyopatikana kupitia elimu, utaalamu wa kitaalamu, na ushirikiano kati ya serikali na taasisi za elimu ya juu, ikichangia juhudi za pamoja za kuokoa maisha ya wanyama.

‎.

‎Kwa sasa, tembo mdogo amerejeshwa katika makazi yake ya asili na kuunganishwa na familia yake huku akiendelea kupata ulinzi na ufuatiliaji wa karibu kutoka TAWA huku afya yake ikizidi kuimarika.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn