logo

MIFUMO BUNIFU YA KITEKNOLOJIA YARAHISISHA SHUGHULI ZA KILIMO SHAMBANI-MANOTA

Wadau wa Kilimo nchini wakiwemo wakulima wametakiwa kutumia teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kupata huduma za Ugani, mapendekezo ya matumizi sahihi ya pembejeo, manunuzi na kuuza bidhaa za kilimo.

‎Wito huo umetolewa na mkulima wa mazao ya bustani kutoka mkoa wa Manyara, Bw. Shaban Manota, alipotoa hotuba yake kama Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa mifumo miwili bunifu ya kiteknolojia.

‎.

‎Kampuni ya MazaoHub ilimtunuku heshima hiyo kutokana na mchango wake mkubwa na mafanikio aliyoyapata kupitia matumizi ya teknolojia za MazaoHub.

‎.

‎Akizungumza na wadau wa kilimo waliojitokeza kwenye Uwanja wa Nane Nane Nzuguni Jijini Dodoma, Manota amebainisha kuwa maendeleo ya teknolojia hiyo yamerahisisha ufanyaji wa shughuli za kilimo huku akisifia ubunifu uliopo katika matumizi kwa njia ya simu kwenye kupata ufumbuzi wa changamoto za kilimo.

‎"Ni wazi kuwa kama wadau wa kilimo wakiwemo wauzaji na wanunuzi bila kuwasahau wakulima wenyewe wakiamua kutumia vema teknolojia basi kilimo kitasonga mbele zaidi ya hapa, mimi ni shuhuda wa matumizi ya teknolojia kwenye kilimo kwa kuwa nilisaidiwa na kampuni ya Mazao Hub inayojihusisha na teknolojia kwenye kilimo." alisema Manota.

‎Mifumo aliyoizindua inayoendeshwa na Kampuni ya Mazao Hub mmoja ni Mfumo Jumuishi wa Kusimamia mashamba ambao ni MazaoHub App na mwengine ni Mfumo Jumuishi wa Masoko ya Mazao uitwao; CropSupply.com.

‎Akizungumzi kwa undani uzinduzi huo Mkurugenzi wa Kampuni ya Mazao Hub, Geophrey Tenganamba anasema kuwa mifumo hiyo ni rafiki kwa kila mtumiaji kuanzia mkulima, wauzaji wa pembejeo, viwanda, wanunuzi wa mazao, Serikali na watumiaji wote huku ikiwarahisishka kufanya kazi zao kwa ufanisi.

‎"Kupitia mifumo ya MazaoHub wakulima, maafisa ugani, wauzaji wa pembejeo (agrovets), wasindikaji, taasisi za fedha na serikali wanashirikiana kwa karibu" alisema Tenganamba.

‎Amesema,"Mfumo unachakata taarifa za Udongo, afya ya mimea , taarifa halisi za mkulima kuwezesha maafisa ugani kumpa mkulima msaada wa karibu kwa kutumia data, Wakulima hupunguza gharama, huongeza mavuno, na hupata masoko pamoja na huduma za kifedha, Agrovets, maafisa ugani, wasindikaji na taasisi zote hunufaika kupitia takwimu zilizothibitishwa na uratibu shirikishi."

‎Tunajivunia mafanikio haya chini ya mpango wa Building a Better Tomorrow (BBT) kama taasisi ya Vijana katika tekinolojia za Kilimo, kwa kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, na Wizara ya Kilimo chini ya Waziri Hussein Bashe.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn