KM MASWI AFUNGUA KONGAMANO LA MSAADA WA KISHERIA LA MWAKA 2025 JIJINI ARUSHA
Mgeni rasmi katika Kongamano la Msaada wa Kisheria la Mwaka 2025, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Eliakim Maswi tayari amefungua rasmi Kongamano hilo leo 23 Julai, 2025 ambapo amesema kuwa Wizara ya Katiba na Sheria imekuwa ikichukua jitihada mbalimbali za Kuboresha utoaji wa huduma ya Msaada wa kisheria ikiwemo kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.
Amesema Kongamano hili ni jukwaa la kitaifa la mazungumzo, tathmini pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha mfumo wa msaada wa kisheria nchini ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidemokrasia.
Kongamano hili linafanyika kwa siku mbili 23-24 Julai, 2025 katika Ukumbi wa Lush Garden jijini Arusha likiea limeratibiwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Maendeleo.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

