logo

WIZARA YA UCHUKUZI TUTAENDELEA KUIMARISHA HUDUMA BORA ZA UCHUKUZI NCHINI -PROF.MBARAWA

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa ameliambia Bunge la Tanzania kuwa Wizara yake kupitia Mamlaka za udhibiti nchini, zimeendelea kuimarisha huduma na ubora wa huduma za uchukuzi nchini ili kukidhi viwango vinavyohitajika kote duniani.

Kauli ya Waziri Mbarawa ameitoa leo Mei 15, 2025 wakati akiwasilisha Hotuba ya bajeti ya Wizara yake kwa Mwaja wa fedha 2025/26 leo Bungeni Mjini Dodoma akizitaja Mamlaka hizo zenye kusimamia huduma za uchukuzi kuwa ni pamoja na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCA).

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn