logo

JUMLA YA MIRADI YA MAJI 2,331 IMEKAMILIKA - WAZIRI AWESO

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema Jumla ya miradi ya maji 2,331 imekamilika ambapo 1,965 ni ya vijijini na 366 ni ya mijini na hivyo kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kutoka wastani wa asilimia 70.1 mwaka 2020 hadi asilimia 83 mwezi Desemba, 2024 na maeneo ya mijini kutoka wastani wa asilimia 84 hadi asilimia 91.6.

.

"Kuanzishwa kwa RUWASA kumejenga miradi 3,379, na kupeleka huduma ya maji katika vijiji 10,517 kati ya vijiji zaidi ya 12,318. RUWASA imefanya mapinduzi makubwa katika kujenga na kuboresha huduma ya maji vijijini.

.

"Baadhi ya miradi iliyokamilika ni awamu ya kwanza ya mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda miji ya Tinde na Shelui; mradi wa ujenzi wa mfumo wa kutibu maji katika Mji wa Bunda; mradi wa ujenzi wa chanzo cha maji Butimba; mradi wa maji Kyaka/Bunazi mkoani Kagera; mradi wa maji katika Mji wa Orkesumet; mradi wa maji Dareda, Singu, Sigino na Bagara mkoani Manyara; na miradi 218 chini ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO 19" alisema Aweso.

.

Waziri Aweso ameyasema hayo leo Mei 08,2025 alipokuwa akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha kwa mwaka wa Fedha 2025/2026 Bungeni jijini Dodoma.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn