PAPA FRANCIS AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 88
Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis, inaripotiwa amefariki dunia leo Jumatatu akiwa na umri wa miaka 88, siku moja baada ya kuonekana akiwa na matumaini katika uwanja wa Saint Peter's Square jana Jumapili ya Pasaka.
.
Kardinali Kevin Farrell amethibitisha kifo cha Papa Francis ambapo taarifa hiyo ilichapishwa na Vatican kwenye chaneli yake ya Telegram.
“Ndugu na wapendwa, ni kwa masikitiko makubwa kwamba sina budi kutangaza kifo cha Baba yetu Mtakatifu Francisko.
"Leo asubuhi saa 7:35 askofu wa Roma, Francis, alirejea nyumbani kwa Baba, Maisha yake yote yaliwekwa wakfu kwa huduma ya Bwana na kanisa Lake."
.
Aidha, Kifo cha Francis kimekuja siku moja tu baada ya kuufurahisha umati wa waumini huko Vatican Jumapili ya Pasaka kwa kuonekana kwenye balcony kwenye Basilica ya Saint Peter licha ya kuwa bado anaendelea kupata nafuu baada ya kuugua vibaya.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

