logo

REA YAWATAKA VIONGOZI WA VIJIJI KUSIMAMIA NA KULINDA MIRADI YA UMEME WALIYOPATIWA

Mkurugenzi wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA)Ndg.Oswald Urassa amewataka viongozi wa maeneo yaliyopelekewa miradi ya umeme kupitia REA kuhakikisha wanaisimamia na kuilinda ipasavyo kwani Serikali imetoa fedha nyingi ili ikamilike na kuhudumia wananchi.

.

Urassa ameyasema hayo Septemba 10,2023 alipokuwa ametembelea miradi ya Umeme katika kata ya Handali wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

.

Amesema miradi ya umeme na maji inatakiwa ilindwe ili kuhakikisha kwamba lile lengo lake la kuletwa kwenye maeneo hayo linafikiwa hivyo amewaomba washirikiane na wananchi pamoja na viongozi husika kwa kuhamasisha ulinzi.

.

"Napenda kutoa ombi kwa viongozi wetu kulinda miradi hii Ili iendelee kuwepo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi husika" alisema Urassa.

.

Aidha, Urassa ameiomba RUWASA wajitahidi kuhakikisha kwamba lengo la kuhakikisha wananchi wote wanapata maji safi linakamilika kwa wakati.

.

Naye Mkurugenzi wa Umeme Vijijini(REA) Mhandisi Jones Olotu amesema miradi hiyo inalenga kwenda kumpunguzia mwanamke changamoto ya kutafuta maji kwa umbali mrefu kupitia kampeni ya kumtua mwanamke ndoo kichwani, hivyo viongozi na wananchi wa kata hiyo wanapaswa kuongeza nguvu katika kujenga matenki ya maji ili waweze kupata Huduma.

.

Mhandisi Olotu pia amesema wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakichimba maji chini jambo ambalo sio sahihi kabisa hivyo miradi hiyo inatakiwa ifanyiwe haraka iweze kukamilika.

.

"Serikali imefanya kutoa Fedha, imeleta wakandarasi ili wananchi wapate maji lakini mikwamo inatokea huku chini, tutaongea na wenzetu wa RUWASA wananchi wapate maji kwa wakati kama ilivyopanga" alisema.

.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Bw.Emmanuel Madali ameishukuru REA kwa kuwapelekea mradi huo wa umeme katika kata yao.

.

Aidha, Madali ametoa wito kwa watumishi wa serikali wanaokwamisha miradi ya serikali wajitahidi kutafuta wakandarasi ambao wapo makini na kazi zao.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn