logo

RC SENYAMULE: KANDA YA KATI IMEJIPANGA KUKABILIANA NA MABADILIKO TABIA YA NCHI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amesema ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo imeendelea kuathiri uzalishaji wa mazao ya kilimo,Mifugo na Uvuvi katika Mikoa ya Kanda ya kati,Mikoa hiyo imejipanga kutoa Mbinu mbalimbali na ujumbe ambao utawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi kuhimili mabadiliko hayo.

Senyamule amesema hayo Leo Julai 31,2023 wakati akizungumza na waandishi wa Habari Kuelekea Sherehe ya maadhimisho ya Nane Nane Kanda ya Kati ambayo yatafanyika katika Viwanja vya Nane Nane jijini Dodoma kuanzia Agosti 01,2023 hadi Agosti 8,2023.

Aidha, Senyamule ameongeza kuwa Maonesho ya Mwaka huu yatakuwa Tofauti na Maonesho ya miaka iliyopita, kwa kuwa yatahusisha matukio muhimu na makongamano yanayoongeza wigo wa uzalishaji bora.

Kauli mbiu ya Maonesho na Sherehe za Nane Nane Kitaifa kwa mwaka 2023 ni; “Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula” na Kaulimbiu ya Kikanda ni “Kilimo ni Biashara, Biashara ni Uwekezaji”.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn