logo

WANANCHI TUMENI VIFURUSHI NA VIPETO KWA WATOA HUDUMA WALIOPEWA LESENI- DKT.BAKARI

Rai imetolewa Kwa Wananchi Wote Kutuma vifurushi na Vipeto Kwa watoa Huduma Ambao wamepewa leseni na TCRA Ili Kupunguza Vitendo Vya wizi Pamoja na Upotevu unaoweza Kujitokeza na kujihakikishia Usalama.

.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabiri Bakari Ametoa Wito Huo Leo Julai 18,2023 Alipokuwa akizungumza Na Waandishi Wa Habari Jijini Dodoma Kuhusu Utekelezaji Wa Majukumu ya Taasisi Hiyo na Muelekeo wake Kwa Mwaka 2023/24.

.

Amesema Sekta Ya Mawasiliano Ya Simu imeendelea kukua Hapa Nchini ambapo Hadi Kufikia Mwezi Juni 2023,kulikuwa Na Laini za Simu Milioni 64.1 Kutoka Laini Milioni 56.7 Sawa na Ongezeko la 13%.

.

"Idadi Hii ya Laini za Simu inahusisha Laini zinazotumiwa na Watu na Laini zinazotumiwa Kwa Ajili ya Mawasiliano Kati Ya mashine kwa Mashine. Aidha Tunawatoa Huduma Sita kwenye Soko" Amesema Bakari.

.

Bakari Amesema Kwa Mujibu wa Tafiti Mbalimbali Hadi Kufikia Juni 2023, Tanzania imeendelea Kuwa Nchi Yenye Kiwango kidogo Sana Cha Bei ya Data Ya GB 1 ukilinganisha na Nchi Nyingine za Afrika Mashariki ambapo Gharama ya GB 1 Ni Dola za Marekani 0.71 Sawa na Shiling 1,666.

.

Mkurugenzi Huyo Amesema TCRA imeendelea kubaini simu za ulaghai zinazoingia hapa nchini na hatua stahiki zimekuwa zikichukuliwa. Kutokana na hatua hiyo, idadi ya simu za udanganyifu imeendelea kupungua kuanzia mwaka 2020 hadi Juni 2023.

.

Aidha,Takwimu za Mawasiliano za Mwezi Juni 2023 zinaonyesha Kwamba Huduma za Pesa Kupitia Simu za Mkononi zimeongezeka, Akaunti za Pesa Kwa Simu ya Mkononi zimeongezeka na Kufikia 47,275,660 Juni 2023, Kutoka Akaunti 38,008,482 Mwezi Julai 2022 ikiwa Ni Ongezeko la Asilimia 24.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn