CGI MAKAKALA AFANYA ZIARA JIJINI ARUSHA
MKUU wa Jeshi la Uhamiaji Tanzania CGI Dkt.Anna Makakala Jana tarehe 11 Julai 2023 amefanya ziara ya kikazi Mkoani Arusha na kuongea na Maafisa na Askari kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi.
Katika Ziara hiyo, CGI Makakala amesisitiza suala la Huduma Kwa wateja, ambapo amewataka Maafisa na Askari kuendelea kutoka huduma bora kwa wateja zinazokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa kwani kufanya hivyo kunasaidia kuimarisha taswira ya Jeshi la Uhamiaji na Taifa Kwa ujumla.
Aidha, Makakala amesisitiza suala la nidhamu, kufanya kazi kwa utii, uhodari na weledi wa hali ya juu sanjari na kuishi katika kauli mbiu ya Uhamiaji Upendo, mshikamano, uwajibikaji na kukataa rushwa.
Akitoa taarifa ya Mkoa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Arusha SACI Joseph Kasike amesema Mkoa huo upo shwari na unaendelea kutekeleza majukumu yake kwa utii, uhodari na weledi wa hali ya juu, ili kufikia Dira ya Jeshi la Uhamiaji na Taifa Kwa Ujumla.
@uhamiajitz
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news