DAMBULANCE 17 TUTAPELEKA KIGOMA KWA AJILI YA KUBEBEA WAGONJWA''KT.MOLLEL ''
NAIBU Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel amesema kuwa, Mkoa wa Kigoma utapata magari ya kubebea wagonjwa 17 (Ambulance) zitazosaidia kutatua changamoto ya huduma za Rufaa na pamoja na vifo vya mama na mtoto katika Mkoa huo.
Mollel amesema hayo alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma.
Amesema Serikali imenunua jumla ya magari ya kubebea wagonjwa 727 ambayo inatarajia kugawa nchi nzima, huku akibainisha kila Halmashauri inatarajia kupata magari mawili na hospitali ya Mkoa kipata gari moja hali itayosaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa magari hayo katika Mkoa.
"Tumenunua Ambulance 727, na tayari Ambulance hizo zimeanza kuingia, na Tumekubaliana angalau zifike Ambulance 200, kuna uwezekano wa kila Halmashauri kupata Ambulance mbili na kila hospitali ya Mkoa kupata Ambulance, hivyo kuna uwezekano wa mkoa wako kupata Ambulance 17 zitazosaidia kupiga hatua katika huduma za Afya." Amesema.
Aidha, Dkt.Mollel amewapongeza Watoa huduma wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni kwa jitihada na ubunifu wanaoendelea kuonesha katika kuboresha huduma kwa wananchi, hali iliyopelekea kupunguza Rufaa za wagonjwa ndani ya Mkoa huo kwa zaidi ya asilimia 28 ndani ya muda mfupi, huku malengo yakiwa kupunguza asilimia zaidi ya 90.
Nae, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni) Dkt.Binaga amesema Hospitali itaendelea kushirikiana na Serikali kuu kutenga fedha kwaajili ya maendeleo ya miradi mbalimbali inayoendelea katika hospitali hiyo ili kuhakikisha inamalizika kwa wakati na wananchi wanaanza kunufaika na huduma katika miradi hiyo.
@wizara_afyatz
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

