logo

MTANZANIA DKT.PEDRO AIBUKA BINGWA ‎KWA KUTWAA TUZO 2 KUBWA ZA MOYO DUNIANI NCHINI MAREKANI

Dkt. Pedro Palangyo, Mtanzania na Mwafrika wa kwanza kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), ameingia kwenye historia baada ya kutwaa tuzo mbili kubwa za kimataifa za utafiti wa magonjwa ya moyo kwa wanawake.

‎Tuzo hizo Dr. Jay Brown International Best Abstract Award na Paul Dudley White International Scholar Award—zimetolewa katika Mkutano wa American Heart Association (AHA) uliofanyika New Orleans, Marekani.

Dkt. Pedro amesema mafanikio hayo ni matokeo ya utafiti wake wa miaka 10 kuhusu Peripartum Cardiomyopathy, ugonjwa hatari unaowakumba wanawake wajawazito au waliopata ujauzito hivi karibuni.

‎Ushindi huu umeipa JKCI, Tanzania na Afrika Mashariki heshima kubwa kimataifa, huku wataalamu wa dunia wakisifu utafiti wake kwa kutoa mwelekeo mpya katika utambuzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wanawake.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn